Sunday, 21 June 2015

Mask ya Yai

Leo tujifunze jinsi ya kutunza ngozi yako kwa njia rahisi na kwa kutumia bidhaa rahisi ambazo zinapatikana katika mazingira yetu tunayoishi na kwa bei nafuu. hapa naongelea mask ya yai ambayo itakusaidia kuweka ngozi yako katika hali ya ung'avu na kuonekana kawa na ngozi ya kitoto. kulitumia yai kama musk inaipa ngozi yako afya,mng'ao, ulaini na kuikinga na chunusi.

Hatua ya kwanza
chukua vyombo viwili, kimoja cha ute na kingine cha Kiini
uwe na kitu kama hiki

koroga vizuri ute wa yai 
futa uso na taulo lenye unyevu wa maji ya moto kiasi
anza kupaka ute wa  yai
kaa nao dakika 15 hadi 30 ukauke, uso uwe kama unakakamaa hivi kisha ufute na taulo lenye unyevu kama la mara ya kwanza

Lishe kwa ngozi inayopatikana katika ute wa yai

Protein
Kurekebisha na kuzipa afya seli za ngozi. Inasaidia kuwa na ngozi imara isiyo na makunyanzi.
Potassium
Kuiweka ngozi kuwa na unyevu nyevu wake unaoilainisha. Inatunza unyevu katika seli za ngozi.
Riboflavin     
Inaondoa kemikali zenye sumu zinazoharibu ngozi na kuleta makunyanzi.
Magnesium
Inakupa ngozi nzuri isiyozeeka na inayong'aa. inapunguza kasi ya ngozi kuzeeka.
Hatua ya Pili
Koroga kiini cha yai
Paka kiini cha yai
Kaa na kiini cha yai usoni kwa dakika 15 hadi 30 mpaka likauke na uso ukakamae kabisa
Safisha uso wako na maji baridi
Futa uso wako vizuri na taulo kavu

Lishe kwa ngozi inayopatikana katika Kiini cha yai
Protein
Kurekebisha na kuzipa afya seli za ngozi. Inasaidia kuwa na ngozi imara isiyo na makunyanzi.
Vitamin A      
Inatibu ngozi kavu na inayokakamaa.
Vitamin B2
Inailinda ngozi yako dhidi ya kemikali za sumu zinazoweza kuichakaza ngozi.
Vitamin B3
Inasaidia kupunguza matokeo ya mzio/allergy katika ngozi yako. Inaipa ngozi unyevu nyevu.
Zinc
Inapunguza kasi ya ngozi kuzeeka. Inatibu chunusi na madoa kwenye ngozi. 

No comments:

Post a Comment